Halmashauri ya Mji Kahama imewapatia Pikipiki maafisa Ugani na watendaji wa Mtaa/Vijiji iili kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Tukio hilo limefanyika leo Tarehe 20.12.2017 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Kahama. Katika maelezo yake wakati wa kukabidhi pikipiki hizo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kahama Mh. Abel Shija amewataka wataalamu hao kutumia vyombo hivyo katika kuwafikia wananchi na kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Jumla ya pikipiki 13 zimetolewa kwa wataalamu hao ambapo 8 ni za Maafisa Ugani na 5 ni za Watendaji wa Mitaa/Vijiji.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa