Machi 8, 2017, Wana Kahama wataungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Afisa Maendeleo ya Jamii Wa Mji wa Kahama Ndg. Robert Kwela amesema kuwa Maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Halmashauri (Uwanja wa Taifa) uliopo Kata ya Majengo Mji wa Kahama kuanzia saa 4 asubuhi na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Fadhili Nkurlu.
Maadhimisho yataambatana na Matukio yafuatayo:
Kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kitaifa kwa mwaka 2017 inasema ‘Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi.’ Kaulimbiu hii inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, kibiashara, upatikaji wa mitaji, masoko na mikopo ili waweze kushiriki kwa usawa, na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji tu.
Aidha, ujumbe wa Kaulimbiu ya mwaka huu imezingatia Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000), na Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu hususan lengo namba 5 kuhusu usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa