Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu amefungua Kikao cha Kamati ya Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Wilaya ya Kahama ambacho kimefanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama mapema leo.
Kikao hiko ni cha maandalizi ya uzinduzi wa Chanjo ya Mlango wa Kizazi unaotarajiwa kufanyika Tarehe 23.04.2018.
"Lengo la kuanzisha Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ni kukinga mabinti wetu kutokana na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake na hivyo kuboresha afya za jamii ya wanawake" Amesema DC
Akiwasilisha mada, Bi. Carol Marcel kutoka Hospitali ya Mji wa Kahama amesema kuwa kansa ya Malngo wa Kizazi inachangiwa na vitu vifuatavyo:
Dalili za Saratani hii ni kutokwa na damu ya hedhi bila mpangilio, kutokwa na damu baada ya kujamiiana, maumivu ya mgongo, miguu na kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa au kukosa hamu ya kula, kutokwa uchafy wa rangi ya kahawia au wenye damu kwenye uke. Dalili mbaya zaidi ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na fistula na uvimbe wa tezi
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa