Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama mapema leo imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Halmashauri ya Mji wa Kahama. Ikiwa Mji wa Kahama imeweza kutembelea na kukagua miradi ya Elimu, Afya na Barabara.
Akiongoza kamati hiyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Mhe. Thomas Mnyongwa amesema kuwa kamati imeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala unaofanywa na Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mradi wa Afya uliotembelewa na Kamati hiyo ni ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Iyenze, Barabara ya Kilomita nne ya Kagongwa-Kidunyashi, Mradi wa Maji Zongomera na Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule za Isagehe Sekondari na Shule ya Msingi Bukondamoyo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa