Kamati ya Kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto ya Halmashauri ya Mji wa Kahama imejengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ili iweze kusimamia majukumu yake ya msingi.
Mafunzo hayo yamefanyika mapema jana Septemba 4, 2019 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa bado kuna wimbi la watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na amebainisha kuwa moja kati ya vyanzo vikubwa ni wazazi na wananchi kutowajibika katika nafasi zao
"Kama mtu unaona huna uwezo wa kulea watoto kumi kwanini uzae? Halafu unakuta mtu ameshamzalisha mwananamke kisha ameona hali ni mbaya anaamua kuiacha familia. Hii ndo inayochangia ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Juzi juzi kuna wazazi wamewaacha watoto yani Baba aliondoka nabkawaacha watoto na Mama wakambo, naye mama wakambo akaamua kuondoka akawaacha watoto peke yao ndio wahangaike kutafuta ridhiki ya kila siku.. Sasa kupitia Kamati hii niwaombe muende mkafanye kazi kwa dhati kabisa ili twende tukaondoe haya mambo" Amesema DC
Kamati hii ipo chini ya Mpango wa Taifa wa Kupinga Ukatili kwa Wanawake na Watoto "MTAKUWWA" na inaundwa na wataalamu, taasisi na wawakilishi wa makundi mbali mbali yakiwemo ya Dini.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na HUHESO Foundation kupitia mradi wa "Mwanamke Amka"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa