Halmashauri ya Mji wa Kahama imemwagiwa sifa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Kwa kuweza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa kiwango kikubwa.
Sifa hizo zimetolewa leo wakati Kamati hiyo ilipokuwa na ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Wilayani hapa.
Akiongoza Kamati hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema kwa niaba ya Chama Tawala kimeridhishwa na Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Mji wa Kahama kwani ndio iliyopo kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama hiko.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na eneo la Viwanda Bukondamoyo, Eneo la Viwanda Chapulwa, Ujenzi wa Kituo cha afya Nyasubi na Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje Hospitali ya Mji wa Kahama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa