Kahama yaadhimisha siku ya kichaa cha mbwa kwa kutoa chanjo
Imewekwa: September 28th, 2018
Leo ni siku maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa/Paka duniani. Halmashauri ya mji wa Kahama kwa kushirikiana na wadau wake inaadhimisha siku hii kwa kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa. Chanjo hii itatolewa kwa siku tatu kuanzia leo hadi tarehe 30/09/2018 kwenye viwanja vya magereza mjini Kahama.Hii ni siku pekee tunakumbushwa kuhakikisha tunautokomeza ugonjwa huu unao athiri mbwa/paka na binadamu kwa kuhakikisha unawapatia mbwa/Paka wako chanjo ya kuzuia kichaa cha mbwa.
Sambamba na hilo mpatie chanjo nyinginezo kadiri ya aina ya mbwa uliyenae, kwa kuwa wanyama hawa wamekuwa na msaada mkubwa katika maisha yetu.
Chanjo/tiba muhimu kwa afya njema ya mbwa/Paka wako ni pamoja na;
1. Chanjo ya kuzuia kichaa cha mbwa/Paka (Rabisin Vaccine
2. D.h.l.p vaccine
3.Dawa ya minyoo(mara moja kila baada ya miezi 3)
4.Vitamini/madini (kutegemeana na aina, umri na lishe ya mbwa).
Kumbuka kutunza kumbukumbu za chanjo ama matibabu ya mbwa/paka wako.