Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo unaofanywa na Manispaa ya Kahama.
Amesema hayo mapema leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi kwenye Manispaa ya Kahama.
Mhe. Ummy ametembelea miradi ya Ujenzi wa Jengo la Kituo cha afya Nyasubi, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje "OPD" Hospitali ya Manispaa, Shule ya Sekondari Nyihogo, ujenzi wa jengo la Ofisi za Manispaa, na Eneo la Viwanda Zongomera.
Pia Waziri amepata wasaa wa kuzungumza na Kamati ya Fedha na Utawala ya Manispaa na Timu ya Wataalamu wa Manispaa ya Kahama "CMT".
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa