Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kahama limekaa katika kikao maalum mapema leo ili kujadili hoja za ukaguzi.
Kikao hicho kilichosimamiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Wajumbe wa Kikao wameweza kutoa maoni na michango yao katika hoja zilizokuwa zinawasilishwa na Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Ndg. Joshua Myaluko kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji.
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2016/17 Halmashauri ilikuwa na Jumla ya hoja 60 kati ya hizo hoja 45 zimefungwa na hoja 15 zimebaki kwa hatua mbalimbali za utekelezaji.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa