Tarehe 14/10/2017 ni siku ambayo Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 zimehitimishwa rasmi visiwani Zanzibar, ambapo Halmashauri ya Mji Kahama imetangazwa kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2017. Akiongea kwa njia ya Simu kutoka nchini Japan ambako yupo kikazi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama, Ndg. Anderson D. Msumba amesema siri kubwa ya Ushindi ni Umoja na Ushirikiano uliooneshwa na Watumishi pamoja na wananchi. "..naamini ni umoja wetu na Watumishi kwa ujumla wetu tulijitoa,lakini pia hata wananchi wengi walituunga sana mkono.
Pili ni aina ya miradi na ubora wake ,kimsingi tukiongeza nguvu nina amini we can do even better" Alisema Msumba.
Mwenge wa Uhuru 2017 ulipokelewa na kukimbizwa Halmashauri ya Mji Kahama mnamo tarehe 15/07/2017 na kuukabidhi Mkoani Tabora Tarehe 16/07/2017
Ukiwa Halmashauri ya Mji Kahama, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa Km 55.8, katika Kata 13, vijiji 2 na mitaa 18 umepitia jumla ya miradi 12 , yenye thamani ya shilingi 6,956,951,494. Ambapo umeweka mawe ya msingi miradi 3 yenye thamani ya shilingi 721,410,000,umezindua miradi 3 yenye thamani ya shilingi 799,664,605, kufungua miradi 3 yenye thamani ya shilingi 268,198,089 na kukagua shughuli/bidhaa miradi 3 yenye thamani ya shilingi 5,167,678,800.Miradi hii ni ya sekta za elimu, Afya, Maji, Barabara, hifadhi ya mazingira, vijana wajasiriamali ,wanawake, mapambano dhidi yaUKIMWI, mapambano dhidi ya malaria, rushwa na madawa ya kulevya.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa