Halmashauri ya Mji Kahama imeunda kamati ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo inaundwa na wajumbe 9 ambao ni:
1. Mkurugenzi wa Halmashauri (Mwenyekiti),
2. Mganga Mkuu wa Halmashuri (Katibu),
3. Afisa Afya wa Halmashauri,
4. Mfamasia wa Halmashauri,
5. Afisa biashara wa Halmashauri,
6. Afisa Mifugo na uvuvi wa Halmashauri,
7. Afisa Kilimo wa Halmashauri,
8. Mweka Hazina wa Halmashauri na
9. Mjumbe mwingine yeyote atakayestahili kuingia katika kamati kwa mujibu wa utaalamu utakaohitajika.
Majukumu Makuu ya Kamati hii ni kama yafuatayo:
1. Kujadili na kuidhinisha maombi ya vibali
2. Kupokea na Kujadili taarifa za ukaguzi na ufuatiliaji
3. Kuainisha shughuli za udhibiti wa vyakula, dawa na vipodozi kama kipaumbele kinachotakiwa kuingizwa kwenye mwongozo wa bajeti.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa