Moja kati ya mambo yaliyowekewa mkazo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kahama ni Suala zima la elimu. Akiongea katika Maadhimisho hayo, aliyekuwa Mgeni Rasmi , Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Fadhili Nkurlu amesema kuwa serikali haitavumilia mtu yeyote atakayesababisha mtoto kutoenda shule. Mtoto yeyote anayestahili kwenda shule anapaswa kwenda.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ameagiza Halmashauri kuwawezesha wanawake katika nyanja za kiuchumi ikiwemo kuwapatia mikopo ili waweze kujiajiri kwa ujasiriamali.
Maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka yaliambatana na kutoa misaada kwa wagonjwa wa wodi ya Wanawake na Wazazi katika Hospitali ya Mji Kahama, Vituo vya watoto yatima na kwa wajane.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa