NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, ameshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, huku akitoa maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuwainua wanawake kiuchumi.
Akiongea kwenye kilele cha Maazimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Iliyofanyika Kimkoa Wilayani Kahama, Mhe. Dugange amewataka wataalamu kutoa mikopo inayotakana na asilimia ya makusanyo kwa usawa na haki.
Allmesema Mikopo hiyo imekuwa ikitolewa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, kwa ajili ya kuinua makundi hayo kiuchumi, na kuonya ukiritimba juu ya utolewaji wa mikopo hiyo.
Aidha Dugange amewapongeza Wanawake wote kwa kuazimisha siku yao kwa hamasa kubwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa