Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha leo ameongoza zoezi la Upimaji wa afya wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani. Akiongea na wananchi waliofika kwenye Maadhimisho hayo Mhe. Macha amewaasa wananchi kuweka mazoea ya kupima afya zao ili waweze kujijua namna ya kuishi salama. Katika hatua nyingine Mhe. Macha amebainisha kuwa tatizo la wadada wanaojiuza "Dada Poa" chanzo kikubwa ni Wanaume kwani ndio wateja wao wakubwa.
"Tusiishie kuwaita hao wanaojiuza 'Dada Poa', nadhani tunahaja ya kuwaita na wanaume "Baba Poa" kwani hao ndio wateja wao, wasipowafuata wanakosa wateja" Amesema Macha.
Desemba 1 ya kila mwaka ni siku ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. Kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama imeadhimisha hii siku kwa kufanya Usafi na kupima afya. Kauli mbiu ya Siku ya Ukimwi duniani Mwaka huu inasema "Ijue Afya Yako: Pima, Jitambue, Ishi"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa