Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ameongoza harambee ya kumchangia Bi. Fatuma Mabanga ambaye ni muathirika wa ukatili wa kijinsia. Harambee hiyo imefanyika mapema leo kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika bwalo la polisi Mjini Kahama.
Kiasi kilichofanyika ni fedha taslimu milioni moja na laki moja, Kiwanja kimoja, Mifuko 10 ya sementi na bati tano. Pamoja na michango hiyo Bi. Fatuma amekabidhiwa kadi ya Benki ya NMB maalumu kwa ajili ya michango mbalimbali kwa watakao guswa.
Sambamba na hilo Umoja wa Mapolisi Wanawake wametoa misaada mbalimbali kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima.
Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia yametanguliwa na maandamano yaliyofanyika kutoka kwenye ofisi za Makao makuu ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kuelekea eneo la bwalo la polisi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa