Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ametoa onyo kwa wafugaji wanaoiachia mifugo yao kutembea mitaani kwani ni kinyume na sheria za Miji.
Ametoa onyo hilo alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa wa Shunu kupitia mkutano wa hadhara.
"Mifugo bado ni changamoto hapa mjini, sasa nawaambia kuwa wafugaji wote ambao bado wanafuga holela na kuruhusu mifugo yao kukatiza mijini tunakwenda kuikamata hiyo mifugo na kuifungia, tunaipa chakula akitoa mwenye nayo atatakiwa kulipia gharama zote na adhabu yavkukaidi sheria na ikifikia wakati mwenye nazo hajajitokeza tunaiuza" Amesema Macha.
Katika hilo Mhe. Macha amemuagiza Mkurugenzi wa Mji wa Kahama kutengeneza zizi la kukusanyia mifugo hiyo ambayo itakamatwa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa