Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa mapambano dhidi ya Virusi vya CORONA yanahitaji zaidi nguvu moja yenye ushirikiano na kujituma.
Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akiongea na wataalamu wa kada mbalimbali wa Halmashauri ya Mji wa Kahama nje ya ukumbi wa Halmashauri.
"Wataalamu mnapaswa kutoa elimu kwa wananchi, na ikitokea mtu haitikii chukua hatua zinazostahili. Hii ni Vita, hivyo kila mtu kwa nafasi yake lazima asimamie kanuni za kujikinga na huu ugonjwa, kama wataalamu tunawajibu wa kutoa elimu na kusimamia sheria". Amesema Macha.
Katika kikao hicho ambacho kilizingatia kanuni zote za kujikinga ikiwemo Kukaa Mita moja baina ya mtu na mtu kiliisha kwa Mhe. Macha kutoa agizo la kuzuia masoko yote ya usiku yasiyo rasmi hadi hapo maelekezo mengine yatakapotolewa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa