Benki ya Posta Tanzania "TPB" Wilayani Kahama imechangia maendeleo ya elimu kwa kutoa Madawati 50 na Viti 50 kwenye Shule ya Sekondari Nyashimbi iliyopo Halmashauri ya Mji Kahama. Makabidhiano hayo yamefanyika Shuleni hapo mapema leo.
Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Masoko wa Benki hiyo Ndg. Henry Bwogi ameitaka jamii kujitokeza kushiriki katika kuchangia maendeleo ya shule.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba ameishukuru Benki ya Posta kwa kujitoa kuchangia maendeleo ya elimu na Pia ametoa wito kwa Wadau wengine kujitokeza kufanya hivyo ingawa amebainisha kuwa Halmashauri kwa nafasi yake imejipanga kuboresha miundombinu ya shule.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa