Timu ya Benki ya Dunia pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mapema leo imefika Halmashauri ya Mji wa Kahama na kutembelea maeneo ambayo yamewasilishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji wa Kahama kuwa yanahitaji usaidizi wa Benki hiyo ili kuweza kuboresha huduma kwa Wananchi.
Miradi ambayo imependekezwa kuingizwa kwenye usaidizi wa Benki ya Dunia ni pamoja na Barabara za kiwango cha Lami, Machinjio ya Kisasa, Dampo la Taka ngumu, Stendi kuu ya Mabasi pamoja na Soko.
Baada ya Kuipitia miradi hiyo yote, timu ya Benki ya Dunia na TAMISEMI kwa pamoja wamekubali kwa moyo mmoja kwamba miradi iliyopendekezwa inakidhi vigezo vya kupewa usaidizi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa