Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Kahama laazimia kuanza kuyatumia majengo yaliyokuwa yanatumiwa na Halmashauri ya Ushetu kwa ajili ya shughuli zake. Maazimio hayo yamefikiwa mapema leo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani robo ya tatu ya Mwaka Januari- machi 2017. Majengo hayo yamekuwa na mvutano wa umiliki kwa muda mrefu baina ya Halmashauri ya Mji Kahama na Ushetu baada ya iliyokuwa Halmashuri ya Wilaya Kahama kuvunjwa.
Hata hivyo Halmashauri ya Ushetu imepokea maelekezo ya kukabidhi majengo hayo kwa Halmashauri ya Mji Kahama na tayari Mkurugenzi wa Ushetu amekwisha kabidhi kwa maandishi majengo hayo licha ya kupata upinzani kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani wake.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa