Baraza la Madiwani Mji wa Kahama limeazimia kuunda tume ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi iliyopo ndani ya Mji wa Kahama. Maazimio hayo yamefikiwa mapema leo kwenye siku ya pili ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani robo ya tatu Januari - Machi 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama. Akitangaza azimio hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kahama Ndg. Abel Shija amesema kuwa tume hii itaenda kubaini changamoto na kupendekeza suluhisho la Migogoro ambayo ni ya muda mrefu na majibu hayajajitosheleza kutoka kwa wataalamu. Aidha ameahidi kuitangaza tume hiyo siku si nyingi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa