Ujumbe wa viongozi watano kutoka Bakhresa Group leo wamefika mji wa Kahama kwa lengo la kupata ardhi ya kuweza kujenga kiwanda cha soda na usindikaji wa matunda. Ujumbe huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ambaye amewashukuru kwa uamuzi huo na kuwahakikishia kuwapa ushirikiano mkubwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa hii ni fursa kubwa kwa Kahama. Msumba ametoa wito kwa wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza wafike Kahama kwani maeneo yapo na kama andiko lipo vizuri eneo linatolewa bure gharama itakuwa ni hati tu.
Bakhresa anahitaji ekari hamsini kwa ajili ya kujenga kiwanda hiko na tayari amekwisha oneshwa eneo hilo. Kama mambo yataenda kama yalivyopangwa baada ya Miezi 18 Kiwanda kitaanza kazi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa