Wana Kahama wametakiwa kutumia muda ulioongezwa wa siku tatu kwa ajili ya kujiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura ili kuweza kupata haki yao ya msingi ya kikatiba ya kugombea na kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 24 Novemba ,2019.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Stephen Magala leo mara baada ya Tamko la kuongezwa kwa siku za uandikishaji lililotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo.
"Kuongezwa kwa Siku 3 za uandikishaji wapiga kura ni fursa muhimu sana kwa Wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha katika Daftari la Orodha ya Wapiga kura aidha kutokana na kutingwa na shughuli zao mbalimbali au kuchanganya zoezi hili na lile la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura lililomalizika tarehe 26/09/2019 Wilayani Kahama. Wananchi ndio chimbuko la Mamlaka ya Utawala wa Nchi yetu ya Tanzania, hii ni kwa Mujibu wa Ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ya Mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho. Kupitia Uchaguzi Wananchi hukasimisha Mamlaka yao kwa Viongozi ili wawawakilishe katika maamuzi mbalimabli ya kutatua changamoto zao mbalimabli ili kujiletea maendeleo. Ni haki kila Mwananchi mwenye sifa kujiandikisha ili apate haki ya kukasimisha Mamlaka yake kwa Viongozi anaowaamini. Shiriki katika Uchaguzi ili kufanya Uamuzi sahihi wa kupata Viongozi watakao kuletea maendeleo usije baadaye kulalamika na haki ya kuchagua umejinyima mwenyewe kwa kutojiandikisha. Mwananchi yeyote timamu Hawezi chezea fursa hii ambayo hujitokeza baada ya miaka 5.Chukua hatua, Fanya maamuzi sahihi upate kushiriki kuchagua Vioongozi bora kwa maendeleo yako" Amesema Magala.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa