• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Habari
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

ACACIA Yakabidhi rasmi uwanja wa Ndege wa Kahama Kwa Serikali

Imewekwa: January 25th, 2018

Kampuni ya madini ya ACACIA yenye kumiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu imekirudisha serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa ujumla.

Awali mwaka 2005 kiwanja hicho kilikabidhiwa kwa makabidhiano maalum kati ya serikali na iliyokuwa kampuni ya madini ya Barrick walioomba ili kurahisisha shughuli zao za migodini ikiwemo ya kutumia ndege kusafirisha wafanyakazi wao na vifaa.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela aliiomba serikali kusaidia kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kutoka Km. 1.5 hadi kufikia Km 2, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa ikiwemo ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400.

“Tunashukuru wenzetu wa ACACIA kwa kurudisha tena serikalini kiwanja hiki, lakini bado tunaimani tutaendeleza ushirikiano baina yetu, lakini ombi langu kwa serikali ni kuongeza urefu wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ili ndege kubwa zaidi ziweze kutua ninaimani zitachochea shughuli za kilimo, biashara na madini na uchumi wananchi utaimarika zaidi,” alisema Bw. Mayongela.

Pia alisema kutua kwa ndege nyingi kutatoa fursa za ajira kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani, ambapo pia TAA itaweza kusogeza huduma zaidi ikiwemo ya maduka, hoteli na mafuta ya ndege, ambapo sasa ndege hazitalazimika tena kujaza mafuta Tabora au Mwanza, kwa safari zake mbalimbali.

Naye Naibu Waziri, Mhe. Kwandikwa alisema serikali itahakikisha inasaidiana na wadau mbalimbali ili waweze kurefusha barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, ili kufanikisha utuaji wa ndege kubwa za abiria na mizigo, ambazo zitachochea maendeleo ya Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

Hatahivyo, Mhe. Kwandikwa aliwataka ACACIA kuweka katika mipango yao ya kusaidia ujenzi wa upanuzi na urefushaji wa Kiwanja cha ndege cha Kahama, ili kiweze kutumika kwa lengo la kutua kwa ndege kubwa, ambapo itachochea sera ya kukuza viwanda.

“Tunamaeneo mengi sana hapa Shinyanga, tunawaita wawekezaji waje kuwekeza kwa wingi katika ujenzi wa viwanda, kilimo, madini na biashara nyingine, sasa usafiri wa uhakika upo ukizingatia tunaviwanja viwili vya ndege kikiwemo hiki cha Kahama na kile cha Shinyanga, na malighafi, umeme na maji vipo vya kutosha hivyo waje tu kuwekeza,” alisisitiza Mhe. Kwandikwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Bi. Telack alisema sasa mkoa wake utainuka kwa kuwa umepata fursa ya kuongezewa kiwanja cha pili cha ndege cha Kahama, ambapo sasa wananchi wataweza kusafirisha mazao ya kilimo na kufanya biashara na mikoa mingine kutokana na usafiri wa ndege ni wa haraka na uhakika.

“Ninakuomba Naibu Waziri najua hili lipo kwenye wizara yako, utusaidie kuharakisha kumalizika kwa kiwanja cha ndege cha Shinyanga, maana hiki hapa tayari kipo ili na sisi tuweze kupata wawekezaji katika viwanda mfano Wachina wasiende kuwekeza mkoani Pwani pekee bali waje na huku, tunaimani tutachochea maendeleo sio ya mkoa wetu tu ila kwa Taifa kwa ujumla,” alisema Bi. Telack.

Kwa upande wa Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu alisema wanajivunia tukio la kurudisha kiwanja cha ndege cha Kahama kwa serikali, ili sasa kiweze kutumika na Watanzania wote katika kuchochea ukuaji wa viwanda.

Hata hivyo, Bw. Busuzu ameahidi wataendelea kutoa huduma mbalimbali kwenye kiwanja hicho kama ilivyokuwa awali, na wataendeleza ushirikiano mzuri ulipo kati yao na TAA.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO June 03, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    May 14, 2025
  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa