Kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa dhahabu wa Buzwagi imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 650,479,914.38 kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha kuanzia Januari - Juni 2018. Makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Akipokea hundi hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Clemence Mkusa amesema kuwa asilimia 60 ya fedha hiyo itaenda kwenye shughuli za Maendeleo mahsusi kwa upanuzi wa hospitali ya Mji wa Kahama ambayo tayari Halmashauri imeshaingia mkataba na Suma JKT kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Akishuhudia makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewaagiza wakurugenzi kuzitumia fedha hizo katika shughuli zilizokusudiwa ili maendeleo yaweze kuonekana.
Mbali na Halmashauri ya Mji Kahama kupokea hundi hiyo pia Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imekabidhiwa hundi ya Shilingi 121,349,478 na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa