Mgodi wa ACACIA Buzwagi imeingia makubaliano na Halmashauri ya Mji wa Kahama juu ya miradi ya ujenzi. Makubaliano hayo yamesainiwa leo kati ya Mgodi na Halmashauri. Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya Makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Mhe. Abel Shija Kishushu ameishukuru Buzwagi kwa moyo wao wa kujitoa katika kuhakikisha jamii inafikiwa na Maendeleo na ameahidi kusimamia makubaliano hayo.
"Binafsi nawashukuru sana kwani mmekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha masuala ya maendeleo mnashiriki. Mmefanya vitu vingi na vinaonekana kwa jamii, na kwa hili la leo pia naamini litasimamiwa kwa umakini" Amesema Mhe. Shija
Katika makubaliano haya ujenzi wa miradi ya elimu ndio imepewa kipaumbele ambapo mgodi utasaidia ujenzi wa madarasa katika baadhi ya shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa