Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Buzwagi umeamua kushirikiana na Serikali katika kupambana na Ugonjwa wa Corona kwa kukabidhi mapipa ya kunawia mikono na kusaidia utoaji elimu kwa umma.
Makabidhiano ya Vifaa hivyo umefanyika mapema leo kwenye Kituo cha Afya Mwendakulima kilichopo kata ya Mwendakulima.
Zaidi ya Mapipa 30 yamekabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Lucas Ngamtwa amewashukuru Barrick kwa Moyo wa kujitoa.
Kwa upande wake Meneja wa Mgodi huo Ndg. Benedict Busunzu amesema kuwa Barrick haiwezi kukaa kimya katika suala la kupambana na Corona kwani hili ni janga la dunia hivyo nao wana jukumu la kushirikiana na Serikali katika Mapambano hayo.
Baadhi ya picha za tukio hilo hizi hapa Chini:
Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi Ndg. Benedict Busunzu akitoa Maelezo wakati akikabidhi Vifaa hivyo.
Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Basil Gervas akitoa neno katika Makabidhiano hayo.
Mganga Mkuu wa Mji wa Kahama, Dkt. Lucas Ngamtwa akitoa shukurani kwa Mgodi wa Barrick .
Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi Ndg. Benedict Busunzu akinawa ikiwa kama ishara ya kufungua matumizi ya mapipa hayo.
Baadhi ya Mapipa ya kunawia yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mganga Mkuu wa Mji wa Kahama Dkt. Lucas Ngamtwa (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi Ndg. Benedict Busunzu baada ya Makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na Corona.
Wataalamu wa Afya wa Mji wa Kahama wakiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Mgodi wa Barrick Buzwagi waliofika katika Makabidhiano hayo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa