Halmashauri ya Mji Kahama leo imefungua rasmi maadhimisho ya wiki ya maji kwa Mkoa wa Shinyanga ambayo yataenda kuhitimishwa tarehe 22/03/2018.
Ufunguzi huu umeambatana na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji katika kata ya Zongomera ambao unagharimu jumla ya fedha za Ki-Tanzania 717,533,397 ambazo ni fedha za ufadhili kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia mradi wa Maji vijijini (Rural Water Supply and Sanitation Program -RWSSP).
Jiwe la Msingi limewekwa na Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mradi huu ukikamilika unatarajiwa kuhudumia watu zaidi ya 19,700. Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Zongomera wameonesha kufurahishwa na mradi huo na kuahidi kuilinda miundombinu kwa nguvu zao zote
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa