Wataalamu wa Idara ya Mifugo na uvuvi Halmashauri ya Mji wa Kahama wametekeza mayai yaliyongia nchini kinyume cha sheria. Uteketezaji huo umefanyika mapema leo kwenye eneo la Dampo la Busoka Mjini hapa. Akiongea wakati wa uteketezaji huo, Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Damian Yustin Kilyenyi amesema kuwa mayai hayo yalikamatwa yakiwa kwenye gari aina ya Fuso mnamo Tarehe 23 Desemba 2018 yakiwa yanatokea nchini Rwanda. Amesema kuwa mhusika alifikishwa kwenye vyombo vya kisheria na amelipa faini ya shilingi laki tatu na kugharamia zoezi la uteketezaji wa mayai hayo.
"Mayai haya yamekamatwa kwakuwa yanatoka nje ya nchi na hayana kibali chochote cha usafirishaji wa mayai hayo, na nchi yetu imezuia uingizwaji wa mifugo au mazao yanayotokana na mifugo ni kwasababu tunataka kujikinga na magonjwa" Amesema Dkt. Kilyenyi.
Aidha Dkt. Kilyenyi amewaasa wafanya biashara wa ndani na wa nje wanaotaka kusafirisha mifugo au mazao yanayotokana na mifugo kufuata sheria na taratibu za nchi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa