Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kanda ya Ziwa zimekaa kikao cha pamoja cha ujirani mwema kujadili masuala ya ulinzi na usalama pamoja na masuala ya maendeleo. Mkoa wa Shinyanga ndio mwenyeji wa Kikao hiko na kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama mapema leo.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Ujirani Mwema ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri amewataka wajumbe kabla ya kuingia kwenye ajenda zao walizopanga ni vyema kujadili suala lililowasilishwa na Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack juu ya uwepo wa udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara dhidi ya bidhaa wanazouza hususan sukari. Wajumbe kwa pamoja wameridhia mjadala huo na kwa pamoja wameibuka na maazimio ambayo wataenda kuyatekeleza.
Awali Mhe. Telack alitoa taarifa ya Oparesheni inayoendelea Mkoani mwake hususan Wilayani Kahama ambapo amebainisha kuwa iwapo Mikoa mingine isipochukua hatua itapelekea kuwa kichaka cha wafanyabiashara wa aina hiyo.
Baada ya mjadala uliohusisha na wataalamu kutoka kiwanda cha Sukari cha Kagera ambao walitoa somo la utambuzi wa bidhaa zao, kikao kimetoa maazimio ambayo kila mkoa utaenda kuyatekeleza.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa