Wadau wanaosimamia masuala ya watoto Mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kuungana na Serikali ya Mkoa katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo imeadhimishwa Wilayani Kahama Kimkoa. Kilele cha Maadhimisho hayo yamefanyika leo Juni 16 2019 kwenye uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Kahama "Uwanja wa Taifa" na mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Wadau wa Mkoa wa Shinyanga ambao ni Mashirika yasiyo ya kiserikali wameshiriki kwa sehemu kubwa Katika kufanikisha siku hiyo kuanzia maandalizi mpaka siku yenyewe.
Katika hotuba yake Mhe. Macha aliitaka jamii kuachana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo aliwasisitiza wazazi kuacha tabia ya kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto wao pamoja na kuwabagua kuwapatia elimu na kufikia hatua ya kuwaozesha ndoa za utotoni wanafunzi wa kike.
Alisema serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayekamatwa akiwafanyia ukatili watoto.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka 2019 inasema “ Mtoto ni Msingi wa Taifa Endelevu, Tumtunze, Tumlinde na Kumwendeleza.”
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa