Mkurugenzi wa Idara ya Elimu TAMISEMI Bw. Julius K. Nestory leo ameendesha mafunzo kwa viongozi wa elimu ngazi ya Halmashauri, Kata na shule kwenye Halmashauri ya Mji wa Kahama. Katika mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Bw. Nestory amebainisha mambo kadhaa katika kuboresha elimu yakiwemo Mambo matano ya ufundishaji wenye ufanisi ambayo ni:
1. Maandalizi kabla ya kufundisha
2. Matumizi
sahihi ya Muda
3. Kufundisha mada kwa kina
4. Kufundisha mada kwa wakati.
5. Tathmini na kukazia Maarifa
"Tunahitaji mabadiliko kwenye elimu.
Sioni vibaya kuona shule imekuwa na walimu wakuu watatu au zaidi ndani ya mwaka mmoja kama lengo ni kutafuta mabadiliko. Na afisa elimu usihofie kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya elimu ya Kahama.
Walimu wakuu mjenge tabia ya kuwapa motisha walimu wanaofanya vizuri shuleni na niwaambie tu Ukitaka ku deal na walimu usichukue wengi, chukua wale ma gangwe deal nao"
Jengeni historia! Mkumbukwe kwenye mazuri.
Utamu wa kutawala ni kufanya maamuzi,
Na Maafisa elimu kata lazima mdhibiti utoro mashuleni.
English speaking policy lazima isimamiwe,
Tunataka kurejesha heshima kwenye elimu
Kuanzia Taaluma, miundombinu, maadili.
Matatizo mawili makubwa ni Usimamizi na ufundishaji usio sahihi, hivyo basi tukikazania haya mabadiliko lazima yafanyike" Amesema Bw. Nestory
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa