• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

Imewekwa: April 16th, 2025

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.
 
Akizungumza jijini Dodoma tarehe 14 Aprili, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari litafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.
 
Ameitaja mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kuwa ni pamoja na Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 01 hadi 07 Mei, 2025.
 
Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 16 hadi 22 Mei, 2025.
 
“Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 28 Juni, 2025 hadi tarehe 04 Julai, 2025,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Ameongeza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo 7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.
 
“Tunatarajia kuwa katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Amesema zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 kinachoipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi mkuu unaofuata.
 
Amesema zoezi hilo litahusisha kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine;
 
Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa  taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
 
Wakati huohuo, Jaji Mwambegele amesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 11(1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume pia ina jukumu la kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura na kuliweka wazi kwa umma.
 
Amesema lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni kutoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa.
 
“Daftari la Awali la Wapiga Kura litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza. Zoezi hili la uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura litafanyika pamoja na uboreshaji wa Daftari wa awamu ya pili,” amesema.
 
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25 Machi, 2025.
Mwisho.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO January 01, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Tangazo la Mikopo ya Asilimia Kumi

    March 28, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa