Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema kuwa baadhi ya askari polisi wa Mji wa Kahama wanahusika na uchochezi wa migogoro ya ardhi inayoendelea Wilayani humo. Amesema hayo mapema leo alipokuwa akiongea na Wananchi wa Kata ya Majengo katika mkutano wake wa Kusikiliza kero za wananchi.
"Kahama ni kinara wa migogoro ya ardhi, na sio migogoro yenye tija, nilikwenda kule Malunga nikaambiwa kuna mgogoro kati ya shule na wananchi, huo mgogoro ulishafanyiwa kazi sana. Lakini kwenye huo mgogoro nimeambiwa kuna watu wanachochea kuni, mgogoro wenyewe halisi haupo isipokuwa kuna watu wapo nyuma ya huo mgogoro na wengine wapo ndani ya Jeshi la Polisi,sasa nataka nitoe onyo, OCD upo hapa, kuna polisi wanachochea mgogoro kwenye eneo la Malunga, nitakupa majina yao naomba uwachukue uwahoji, na nimesema waache mara moja kugombanisha Serikali na Wananchi wake". Amesema Telack
Katika mkutano huo, mkuu wa Mkoa aliongozana na viongozi wa mashirika na Taasisi za Umma zote ili zijibu na kutoa maelezo kwa masuala yote yaliyohojiwa na wananchi.
Kero za Migogoro ya Ardhi ndio zimeongoza kuhojiwa na wananchi. Kero zingine ni za Miundo mbinu ya Barabara na mitaro, Kodi za TRA na Halmashauri, Ongezeko la gharama za kulipia Maji, Umeme usio na uhakika.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa