Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa onyo kali kwa Wanaharakati wanaojificha kwa mwavuli wa Umoja wa Wazee kuleta uchochezi na vurugu kwenye masuala ya msingi. Onyo hilo amelitoa mapema leo alipokuwa akiongea kwenye mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Kata ya Majengo Wilayani Kahama.
"Mkoa wetu unalo baraza la Wazee linalotambulika kisheria, watu wengine wanaowaambia wana baraza la Wazee wanawadanganya, kazi ya wazee ni kushauri sio kupambana na Serikali, ukishakuta kuna wazee wamekuwa wanaharakati ujue kuna tatizo, naomba msiwasikilize" Amesema Telack
Aidha katika mkutano huo Mhe. Telack ameweza kusikiliza kero za wananchi na kuruhusu wakuu wa Taasisi alioambatana nao kuzitolea ufafanuzi papo hapo ikiwa pamoja na kutoa maagizo kwa yale masuala yaliyoonekana yana suasua.
Baadhi ya Kero zilizowasilishwa na wananchi ni pamoja na Miundombinu ya barabara, Migogoro ya ardhi, Kukatika kwa umeme mara kwa mara, Ukadiriaji wa kodi za mapato, Utendaji wa askari wa usalama barabarani na upandaji wa bili za maji kwa watumiaji.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa