Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde amewaahidi wafanyabiashara wa mbao waliopo eneo la Bukondamoyo maarufu kama 'Dodoma' Wilayani Kahama kuwa atamuagiza katibu mkuu wake afike Kahama na kujionea kasi iliyopo na ikiwezekana aweze kupanga kufanya maonesho ya Mifuko kwenye eneo hilo. Ameyasema hayo mapema leo akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilayani hapa.
Mhe. Mavunde ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda na kujionea shughuli zinazofanywa hapo na kusema kuwa kitendo cha Halmashauri ya Mji Kahama kutenga eneo hilo ni hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi.
"Chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tuna Baraza la uwezeshaji kiuchumi, baraza lile tuna mifuko zaidi ya kumi na tisa ambayo inafanya kazi ya kuwezesha wananchi kiuchumi,kuwapa mikopo na kuwapa ruzuku,tumeshakubaliana na mkuu wa mkoa kwamba namimi nita muagiza katibu mkuu wangu wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi afike eneo hili ili aone namna ya kuweza kufanya maoneshomadogo ya mifuko yote mfahamu fursa zilizopo ili kila mmoja kwa nafasi yake aweze kuona atapata fedha wapi za kuinua biashara yake" Amesema Mhe. Mavunde
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa