• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Habari
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

Mkurugenzi Kahama atimiza ahadi yake, atoa Pembejeo kwa vijana wenye nia ya kujiajiri katika Kilimo

Imewekwa: January 24th, 2019

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba ametimiza ahadi yake aliyoitoa Juni 2018 ya kuwapa msaada wa pembejeo vijana wote wenye nia ya kujiajiri katika Kilimo. Ahadi hiyo ameitimiza leo baada ya vijana 28 kujitokeza na kupewa pembejeo zenye thamani ya Sh. Milioni 14.

Akikabidhi pembejeo hizo kwa Wakulima, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa vijana wengi wanashindwa kutumia fursa hiyo waliyopewa na wamekuwa wazembe wa kujiajiri. Amebainisha  kuwa vijana wanapenda kupoteza muda wao kwenye 'kubeti' badala ya kujishughulisha na Kilimo.

Mhe. Macha ameitaka Halmashauri kuwa ifikapo tarehe moja mwezi wa pili kama vijana hawajajitokeza basi fedha zilizokuwa zimetengwa katika bajeti ya 2018/2019 ya kuwawezesha vijana kwenye kilimo wapewe wazee wenye uwezo wa kufanya kazi badala yao.

Aidha Mkurugenzi wa Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amebainisha kuwa tatizo la Vijana kutojitokeza kuchukua ruzuku hiyo ni kwamba wengi wao wanataka wapewe pesa badala ya pembejeo.

Msumba amesema kuwa vijana ukiwapatia pesa huwa urejeshaji wake unakuwa mgumu na ndio maana Halmashauri ya Mji wa Kahama imeamua kutoa pembejeo za Kilimo ili mwenye nia ya kulima apewe. 

Halmashauri ya Mji wa Kahama mwaka wa fedha 2018/2019 imetenga jumla ya shilingi milioni 53.4 kwa ajili ya kuwaptia ruzuku vijana wanaojishughulisha na Kilimo lakini hadi sasa Shilingi Milioni 14 pekee ndio zilizotolewa kwa vijana 28 waliojitokeza na kuonesha nia ya kujikita kwenye kilimo.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO June 03, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    May 14, 2025
  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa