Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba ameridhishwa na kazi zinazofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Farm Concern International ndani ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Amebainisha hayo leo alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
"Hawa Farm concern wanafanya kazi yetu ambayo ilipaswa kufanywa na wataalamu wetu hivyo wamekua msaada mkubwa kwa halmashauri na wanataoa mafunzo yenye tija.
Mkulima anatakiwa kulima apate na ziada na sio chakula peke yake" Amesema Msumba.
Aidha Msumba ameongea na wanufaika wa kazi za shirika hilo ambao wameonesha mwitikio mkubwa na kuonesha kubadilika kulinganisha na hali zao za awali.
Moja kati ya wanufaika hao ni Bi. Sara Maige mkazi wa kijiji cha Bumbiti ambaye ni binti mwenye Elimu ya kidato cha NNE aliyeamua kujiajiri kwenye Kilimo. Ameonyesha uwezo wa kujituma hadi kumfanya Mkurugenzi kumpa motisha ya Fedha (haijulikani kiasi) na kumuahidi kumpatia ruzuku za pembejeo za Kilimo msimu ukianza kwa kuwaagiza Maafisa Kilimo na Maendeleo ya Jamii wamuweke kwenye mpango.
Farm Concern International kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama wamejikita kwenye kuwanyanyua Wakulima kwa kutoa elimu na kuwawezesha rasilimali muhimu za kilimo na kuwasimamia. Kwasasa wanafanya kazi kwenye Vijiji vinne ambavyo ni Chapulwa na Mwendakulima (Kata ya Mwendakulima), Bumbiti na Sangilwa (Kata ya Mondo)
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa