Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshughulikia haki za binadamu na taasisi za dini waombwa kushirikiana na serikali katika kuelimisha jamii kuhusu haki za mtoto na kushiriki kikamilifu katika kuimarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto ili kuwa na maendeleo endelevu. Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya Ya Kahama Ndg. Fadhili Nkurlu aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Kimkoa.
Aidha katika taarifa iliyoandaliwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama iliyowasomwa Kwa mgeni rasmi inaonesha kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama ina mikakati mbali mbali iliyojiwekea katika kumlinda mtoto kwa kuhimiza na kuendeleza haki zake za msingi.
Mikakati hiyo ni pamoja na:
1. Kuendelea kusimamia, kuelimisha jamii na kuhakikisha mtoto anapata haki yake ya kuishi.
2. Kuendelea kuelimisha jamii kuhusu dhana ya mtoto na kuwathamini watoto wao kama hazina ya baadae.
3. kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na unyayasaji na ukatilia dhidi ya watoto na wanaotelekeza watoto wao.
4. Kuendelea Kuelimisha jamii na hasa wazai kuwathamini watoto wao kama hazina kwa maisha yao ya baadae.
Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu 2017 ni "Maendeleo endelevu 2030; Imarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto"
Siku hii ni muhimu sana kwa jamii ya Kitanzania kwakuwa inatoa fursa ya kukumbushana kutetea, kulindana kusimamia haki, usawa, ulinzi na maswala yote
yanayohusiana na Maendeleo ya mtoto. Pia kubaini na kuchambua matatizo yanayowakabili watoto kwa lengo la kuyatolea ufumbuzi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa