Ushirikishwaji wa Jamii katika masuala ya Maendeleo ni moja kati ya nyenzo kubwa sana katika kuyafikia Malengo. Kwa kulitambua hilo,Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Kahama kupitia idara ya Ardhi Mipango Miji na Maliasili itafanya upimaji shirikishi kwa kurasimisha makazi holela (Urban upgrading) katika Kata ya Kagogwa katika vijiji Vya Kagongwa,Kishima,Iponya Na kuukipanga Kijiji cha Gembe,mapema wikii hii wamefanya mikutano ya hadhara katika vijiji vyote vinne kwa nyakati tofauti wakitoa elimu juu ya umuhimu wa zoezi hilo la upimaji, Akiwa anawasilisha mada ya upimaji na umilikishaji Afisa Ardhi Ndg. Lewis Luitbold Milanzi amewataka wananchi kutoa ushirikiano pindi wapimaji watakapokuwa wanatekeleza zoezi hilo na pia kutambua mipaka ya Maeneo yao pamoja na kuyatambua Yale maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za Jamii kama masoko, zahanati,shule, barabara pamoja na maeneo ya wazi ili kuepusha migogoro wakati wa zoezi la upimaji litakapoanza wiki ijayo ambapo zoezi hili litaanza katika Kijiji cha Iponya.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa