Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amewataka viongozi wa Kijiji cha Ntungulu Kata ya Kilago kuhakikisha wanajenga maboma ya nyumba za walimu haraka iwezekanavyo ili akamilishe ujenzi kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha. Agizo hilo amelitoa alipotembelea Shule ya Msingi Ntungulu na Kujionea mazingira magumu wanayoishi walimu wa shule hii.
"Kimsingi ili elimu iwe nzuri ni lazima kwanza kuangalia mazingira ya mwalimu, mwalimu asipokuwa na mazingira mazuri tusitegemee miujiza kwenye elimu.. jengeni maboma hata manne ya 'Two in One' ili tuweze kumalizia hizi nyumba kabla huu mwaka wa fedha kuisha" Amesema Mkurugenzi Msumba.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kilago Mhe. Peter Emmanuel amemuhakikishia Mkurugenzi kuwa watafanikisha unyanyuaji wa Maboma hayo kwani tayari wana ratiba ya kukutana na wananchi ili kuwashirikisha hilo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa