Halmashauri ya Mji wa Kahama yatenga zaidi ya ekari 2600 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. Haya yamesemwa na Mkurugenzi wa Mji Kahama Ndg. Anderson D. Msumba wakati wa ziara ya kukagua Viwanda vikubwa na vidogo na fursa za uwekezaji iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack Wilayani hapa.
Aidha mkuu wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Viwanda katika maeneo hayo kwani yana mazingira rafiki ya kibiashara.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa imeweza kufika maeneo ya Zongomera ambapo ndio kuna eneo lililotengwa kwa ajili ya Viwanda, pia ametembelea viwanda vya uchambuaji wa Pamba vya Fresho, NIDA NA KOM ltd.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa