Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Intra-health wameendelea kutoa elimu ya Tohara kwa hiari kwa wanaume. Kikao cha uhamasishaji huduma ya Tohara kwa wanaume kimefanyika tarehe 13/06/2019 kikiwa na lengo la kuweka muitikio wa jamii katika kufanya tohara ya hiari kwa wanaume ili kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Akiwasilisha mada katika kikao hiko, Mratibu wa masuala ya Tohara Mkoa wa Shinyanga Bw. Msafiri Swai amesema kuwa madahara yanayotokana na kutotahiri ni makubwa hivyo amewataka wanaume kufanya tohara ili kuepukana na kadhia hizo zikiwemo za UKIMWI na Kansa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa