Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu mapema leo amezindua kampeni ya upandaji miti katika Mgodi wa Mwime uliopo Wilayani hapa. Akiongea katika uzinduzi huo Mhe. Nkurlu amewaasa wananchi kuitunza hiyo miti kwani ni jukumu la kila mtu.
Jumla ya miti 500 imepandwa katika uzinduzi wa kampeni kwenye mgodi huo leo. Huku DC akiahidi kuleta miche mingi zaidi eneo hilo.
Aidha katika taarifa iliyosomwa na Ndg. Shadrack Nyamhokya kwa niaba ya wafanyakazi wa mgodi huo, imebainisha changamoto ya uwepo wa wavamimizi wa maduara ambao wamekuwa tishio wa usalama wa wachimbaji katika mgodi huo.
Akijibu changamoto ya Usalama, Mhe. Nkurlu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kahama amewataka wananchi waishio katika maeneo ya migodi midogo kuhakikisha wanaripoti kwa vyombo vya ulinzi na usalama matukio yote yanayoashiria uvunjifu wa amani katika maeneo yao.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa