Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ameagiza kuwa suala la usafi kwa sasa liwe la kilasiku badala ya kusubiri kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuweka mazingira safi.
Agizo hilo amelitoa mapema leo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira yaliyofanyika kawenye viunga vya National housing mjini Kahama.
Macha amesema kuwa suala la usafi bado sio la kuridhisha na kuwataka wafanyabiashara na wananchi kufanya usafi kila siku badala ya kusubiri jumamosi ya mwisho wa mwezi.
"Hali ya usafi katika mitaa ya Kahama sio ya kuridhisha, kwahiyo natoa maelekezo kwa kila mfanyabiashara kila siku kufany ausafi mbele ya eneo lake mita kumi na kuwa na chombo kikubwa cha kuhifadhia taka" Amesema Macha
Mhe. Macha ameishukuru Serikali kwa kuliona tatizo la mifuko ya plastiki katika kuchafua mazingira na kupongeza wananchi wilayani hapa kwa kuitikia wito kwenye agizo la kusitisha matumizi ya mifuko hiyo na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano.
Maadhimisho haya hufanyika kila ifikapo tarehe 5 Juni, ila kwa Kahama mwaka huu imeadhimisha tarehe 7 Juni kutokana na tarehe 7 kuingiliana na ya Sikukuu ya Idd El Fitr
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa