• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Habari
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

CRDB Kanda ya Magharibi yatoa msaada wa madawati Shule ya Sekondari Kitwana.

Imewekwa: October 7th, 2020

Benki ya CRDB kanda ya magharibi imetoa msaada wa viti na meza 88 katika shule ya Sekondari Kitwana Wilayani Kahama mkoani Shinyanga ikiwa ni muendelezo wa kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Jumatatu Octoba 5 mwaka huu. 

Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya kahama Anamringi Macha ameishukuru benki ya CRDB kwa kujitoa mara kwa mara kuchangia miradi ya maendeleo na kuziomba taasisi zingine kuiga mfano wa CRDB.

Macha ameongeza kuwa msaada huo wa viti na meza umepunguza kwa kiasi kikubwa kero iliyokuwepo katika shule ya Sekondari Kitwana  licha ya kwamba mwakani halmashauri  ya mji wa kahama ina mzigo mkubwa kutokana na wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza kuwa wengi kuliko mwaka huu.

Kwa upande wake Meneja biashara wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amesema kuwa msaada huo wa viti na meza umegharimu Shilingi milioni saba na kwamba Benki ya CRDB itaendelea kutoa misaada ya kijamii kupitia asilimia moja ya Faida wanayoitenga kila mwaka.

Sambamba na hayo Wagana ametoa wito kwa wadau na wananchi mbalimbali kuitembelea benki ya CRDB ili kujifunza mengi na kufungua Akaunti mbalimbali kupitia wiki ya huduma kwa wateja.

Naye meneja wa CRDB Tawi la Kahama Evod Kereti amewaasa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitwana kuwa kuna akaunti maalumu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ambayo kufungua ni bure na kwamba wakawaambie wazazi wao ili waweze kuwafungulia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kitwana Flora Cleopa Mwanri amewaomba wadau wa elimu kupitia Ofisi ya mkuu wa wilaya kusaidia upatikanaji wa Bweni la wasichana ili kuwaepusha mabinti na vishawishi vya ngono pamoja na kuwafanya wazingatie masomo.

Awali akisoma Risala mkuu wa Shule ya Sekondari Kitwana Basil Kijazi ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo na kuongeza kuwa kwa sasa kinachowakabili ni thamani za walimu kwani walimu wanatumia viti na meza za wanafunzi.

Benki ya CRDB imeendelea kusaidia misaada mbalimbali ya kijamii ikewemo Afya na Elimu kupitia asilimia moja ya Faida wanayopata kila mwaka katika matawi yake yote nchini.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO June 03, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    May 14, 2025
  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa