MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara
ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili
timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la
kufanyia biashara linalokubalika kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali
kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN 2110 kikamilifu na
kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of
Incorporation or Registration).
(ii) “Memorandum and Article of Allocation” kama ni Kampuni
(iii) Kitambulisho cha mpiga kura, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya
kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi
nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (prowess of a Honey) kama wenye hisa wote
wa Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara
(Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za
malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali , Kwa mfano (TFDA,
EWURA, TAURA, CRB, TILLI) n.k
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa